May 25, 2016

Haya Hapa majibu ya Harmonize kuhusu kumkejeli wema kutoa mimba......Wema anena mazito - video

VIDEO ambayo inawahusisha baadhi ya wasanii wa Kundi la WCB, akiwemo Harmonize wakimkejeli staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu jana ilichafua hali ya hewa na kuzua sintofahamu mitandaoni. Baadhi ya maneno katika video hiyo yanasema; “Sister duu usitoe mimba kesho ulie kama Sepetu”.

Video yenyewe ipo hapa;


Baada ya video hiyo kusambaa kwa kasi mitandaoni, Wema aliamua kuibuka na kutupia picha yake akiwa na mama yake na kuandika haya; “Ipo siku na mimi nitaitwa mama”.

Wema Sepetu

Mashabiki wa Wema walionekana kumsapoti staa huyo na kumponda Harmonize kwa kitendo hicho alichokifanya akiwa na wenzake.
Baada ya sintofahamu hizo, Harmonize aliibuka na kujibu baadhi ya tuhuma hizo akisema video hiyo imevuja bahati mbaya.

Paparazi blog
ONEKANA MJANJA: SHARE HABARI HII KWA MARAFIKI ZAKO NA KATIKA MAGROUP YA WHATSAPP FREE (only for mobile)

TUPE MAONI YAKO HAPA!