May 25, 2016

AIBU: binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe agoma kumpa mkono Paul Makonda wakati wa kuuaga mwili wa marehemu

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akiweka shada la maua katika jeneza la Marehemu Wilson Kabwe aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji
Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akiweka shada la maua katika jeneza la Marehemu Wilson Kabwe aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji
ANNA Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkono Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.
Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.
Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.
Kabwe amefariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauti yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipo kuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike.

Paparazi blog
ONEKANA MJANJA: SHARE HABARI HII KWA MARAFIKI ZAKO NA KATIKA MAGROUP YA WHATSAPP FREE (only for mobile)

TUPE MAONI YAKO HAPA!