May 25, 2016

Iko siku na mimi ntaitwa Mama – Wema Sepetu

Wema Sepetu ana kila kitu anachokitaka duniani, fedha, magari na vingine lakini amekosa kitu kimoja tu muhimu – mtoto.
13257005_1158301677555796_27744686_n
Na Miss Tanzania huyo wa zamani anataka watu wajue kuwa suala la mtoto si kitu anachokichukulia poa hata kidogo. Muigizaji huyo alielezea hisia zake hizo kwa kupost picha akiwa na mama yake na kuandika: Iko siku na mimi ntaitwa Mama.’ Aliongeza emoji za mtu mwenye huzuni.
Miezi kadhaa iliyopita Wema na Idris walitangaza kutarajia kupata watoto mapacha lakini baadaye walitangaza kuwapoteza. Kwa muda mrefu Wema amekuwa muwazi kuhusu tatizo lake la kutoshika mimba katika muda anaotaka kufanya hivyo.
Mashabiki wake wameendelea kumpa moyo na kumtaka asikate tamaa.
“Usikate tamaa @wemasepetu unakumbuka sara wa ibrahim alizaa akiwa mzee sana cha msingi endelea kumwomba mungu na jiweke karbu nae hakuna kinachoshindikana kwake,” ameandika shabiki mmoja.

Paparazi blog
ONEKANA MJANJA: SHARE HABARI HII KWA MARAFIKI ZAKO NA KATIKA MAGROUP YA WHATSAPP FREE (only for mobile)

TUPE MAONI YAKO HAPA!